Miezi michache tangu ahamishie makazi yake nchini Afrika Kusini, modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametia aibu kutokana na kudaiwa ‘kujiuza’ kwa njia ya mtandao nchini humo.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo kimedai kuwa, Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.
“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao, si unajua tena mtoto kajaliwa shepu la maana.
“Ukitaka kuthibitisha hilo ninalokwambia, ingia katika akaunti yake utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini, kama siyo kutuaibisha na kujiaibisha mwenyewe ni nini?” kilihoji chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kuvujisha habari hiyo, mwandishi wetu aliingia kwenye akaunti ya mrembo huyo na kujionea picha kibao zenye mapozi ya kihasara.
0 comments:
Post a Comment