Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kuwa ndani ya tasnia yao, kuna wasanii wengi wa kike wanajiuza kwa maslahi yao binafsi.
Akiongea na Gpl, Davina alisema wasanii wanaofanya hivyo ni wale wasio na nia ya dhati, wapo kwenye tasnia kwa ajili ya kuuza sura na kujinadi kwa mapedeshee.
“Tatizo ni kwamba wasanii tumekutana kila mmoja ana tabia zake na ni ngumu kujua undani wa mtu kwa kumtazama mara moja, sasa utakuta mtu yupo radhi aombe kucheza filamu hata bure kwa kuamini kwamba ataonwa na wanaume wenye pesa zao, na kweli inakuwa hivyo kwani wanapowatokea hawakatai, kimsingi wanatuchafua sana sisi ambao tupo serious na kazi,” alisema Davina
0 comments:
Post a Comment