MSANII WA FILAMU ALIA NA KUSEMA: WOLPER KANIPORA DEMU WANGU, WOLPER AFUNGUKA




Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
MSANII wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kumchukua mpenzi wa msanii wa filamu ambaye pia ni mpigapicha, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’ aliyejulikana kwa jina moja la Vivian.Chanzo cha habari kililiambia kuwa, tangu Wolper awe karibu na Vivi, Farid amekuwa akiumia sana kwani amekuwa akikosa muda wa kujiachia naye.

“Yaani Wolper kampora Farid Vivi wake, sasa hivi jamaa ameamua kumuacha maana anaona mambo hayaendi sawa.

“Watu wanajiuliza, Wolper anampa nini Vivi? Ni ushosti wa kawaida tu au kuna kingine. Maana mtu huwezi kumuacha mpenzi wako kisa msichana mwenzako,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Mpenzi wa ‘Farid Uwezo’,Vivian.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Farid na alipopatikana alisema ni kweli Vivi alikuwa mpenzi wake lakini Wolper kampora.
“Vivian alikuwa ni mpenzi wangu lakini baada ya kuwa na urafiki na Wolper alibadilika na kunikataa.
“Nilishindwa kujua sababu ya yeye kutotaka kuwa na mimi kwa kuwa Wolper ni msichana mwenzake. Inaniuma sana kwani nilikuwa nampenda sana, hata hivyo siwezi kumrudia kwani atakuwa ameshaharibika kitabia,” alisema Farid.


Msanii wa filamu Bongo, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’.
Alipotafutwa Wolper kuzungumzia madai hayo alisema, anashangazwa na taarifa hizo na anachokijua yeye ni kwamba Vivian ni rafiki yake Farid ni mtu wake.
“Kwanza Farid ni mtu wangu wa karibu sana ambaye sidhani kama anaweza kusema maneno hayo. Pili Vivian ni rafiki yagu wa kawaida, mimi nadhani kuna maadui zangu wanataka kunichafua,” alisema Wolper.
-GPL
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment