Uwoya Asema Yupo SERIOUS Kuhusu Mipango ya Ndoa na Mwimbaji Jaguar wa Kenya


Udaku Special Blog: Mwanadada Irene Uwoya amesema ingawa Jaguar alishindwa kuja kuzungumza na wazazi wake kuhusu ndoa yao, bado wanawasiliana vizuri na kila kitu kipo sawa.
Akizungumza na Mpekuzi, Irene amesema mahusiano yake na Jaguar yapo japo hajafanya maamuzi ya kuolewa.

“Jaguar hakuja kuna vitu ambavyo vilitokea vikasababisha asije,”amesema mrembo huyo.

“Kila siku naongea naye na uamuzi wake upo pale pale. Mimi mwenyewe bado sijafanya maamuzi ya kusema niolewe lakini akija ndo tutaongea kila kitu.”

Haya hivyo Irene amesema hawezi kuzungumzia ndoa yake na mcheza soka wa Rwanda, Ndikumana waliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Krish.

“Sasa kuhusu hilo nisingependa kuliongelea, mimi nadhani sijui hata nisemeje, sipendi kuongelea mambo yangu binafsi.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment